Waziri wa Uchukuzi wa Kenya Kipchumba Murkomen hivi karibuni aliikosoa vikali Rwanda kwamba “inatawaliwa na mtu mmoja” na ni nchi “ndogo,” kauli iliyoibua hisia tofauti.
Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, CENI, iliongeza muda wa kupiga kura katika baadhi ya maeneo hadi jana Alhamisi.
Viongozi wa nchi za Afrika walikutana nchini Kenya mwezi Septemba 2023, katika Mkutano wa Afrika wa Mabadiliko ya Tabia nchi ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake kwa ajili ya kupaza sauti ya bara.
Huku wagombea 26 wa urais wakiwa wamesajiliwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI), Uchaguzi Mkuu unaendelea kutawaliwa na hila na hesabu za vyama vikuu vya kisiasa na miungano inayosukuma pembezoni mwafaka wa msingi wa raia kote nchini.
Serikali ya Tanzania imesema itagharamia gharama za mazishi huku idadi ya majeruhi ikipita watu 80 kufuatia mafuriko ya Katesh wilayani Hanang, mkoani Manyara.
Mwaka 2023 utakumbukwa kwa mingi, lakini kubwa ni mauaji ya kutisha yaliyotokea pwani ya Kenya katika msitu wa Shakahola ambapo mamia ya waumini wa dhehebu la Good News International Ministry walipoteza maisha baada ya kukaa muda mrefu bila chakula.